Usingizi
- Neema Komba
- 3 days ago
- 1 min read

Wanikosesha usingizi
Tanzania ya siku hizi,
Uloikata mizizi
Na kusahau misingi
Uliyosimika siku nyingi
Â
Ndotoni unanijia
Kwa kilio na hasira
‘Nisuta kukosa dira
Na kunidai uhuru
Ulopigania siku nyingi
Â
Wanikumbusha amani
Haiji bila ya haki
Na ukombozi wetu thabiti
Haukuja bila ya dhiki
Na damu za wafianchi